

Msanii wa kizazi kipya hapa nchini Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz usiku wa jana alikuwa akitumbuiza katika kusherekea miaka 10 katika muziki wa Bongo Fleva Mkoani Kigoma ambapo akiwa jukwaani alipigiwa simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt John Pombe Magufuli kisha kupongezwa kwa jitihada zake anazofanya katika sanaa na Taifa kwa ujumla.
Ilikuwa majira ya saa 7:54 usiku akiwa amemaliza kuimba wimbo wa Tetema na Rayvany, ambapo simu hiyo ilipelekwa jukwaani na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akiongozana na meneja wake Babu Tale.
Baada ya kuipokea aliwatangazaia mashabiki waliofika uwanjani hapo kwamba ‘Wanakigoma nimewaambia kitu si nimewaambia leo mna bahati sana, kwenye simu tuko na Mheshimiwa Magufuli piga shangweeee, Mheshimiwa shikamooo.
Baada ya hapo akaweka sauti kubwa ambayo ilikuwa ikisikika kwenye spika, na kumwambia nakutakiwa wewe heri ya mwaka mpya pamoja na Wanakigoma wote, wakati huo mashabiki wakawa wanapiga kelele za babu!babu!babu!.
Kutokana na hali hiyo Diamond aliwatuliza, lakini bado hawakusikia na kuendelea kupiga kelele. Rais amesema alitamani na yeye angekuwepo hapo, lakini amemtuma Polepole na wengine waliokuja hapo.
Diamond alimjibu baba watu tunakupenda sana na tunakuhakikishia awamu inayokuja unapita kwa kishindo sana, tunapiga mia kwa mia, Magufuli oyeeee!CCM oyeee!.
==>>Tazama hapo chiniRais Magufuli apiga simu moja kwa moja stejini kwa @diamondplat akiwa jukwaani, Kigoma yageuka shangwe tupu.#TUNATEKELEZA2019#TUMEAMUA2019 ) January 1, 2020
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527
Malunde 1 blog Ipo PlayStore….Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..